IQNA

Mchezaji wa Chelsea ajenga msikiti Senegal

18:20 - May 10, 2014
Habari ID: 1405411
Demba Ba mchezaji wa Timu ya Soka ya Chelsea katika ligi ya Premier nchini nchini Uingereza amefadhili kikamilifu ujenzi wa msikiti katika nchi yake asili, Senegal.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari za Qur’an la Kimataifa IQNA, Demba Ba mchezaji mashuhuri wa Chelsea amegharamia ujenzi wa msikiti uliopewa jina la ‘Masjid Nasrullah’ katika kijiji cha  Doondu nchini Senegal.
Vyombo vya habari Senegal vimeripoti kuhusu mchango wake huo kabla ya kufunguliwa msikiti huo adhimu katika kipindi cha siku chache zijazo. Demba Ba ni mchezaji mashuhuri  Mwislamu nchini Uingereza ambaye husherehekea mabao aliyofunga kwa kusujudu katika ardhi na kumshukuru Mola. Mchezaji huyo wa Chelsea anasema alilelewa katika familia yenye kufuata misingi ya dini ya Kiislamu.
“Kuwa Mwislamu ni muhimu kwangu mimi zaidi ya kuwa mchezaji. Mwislamu mzuri huwa na shakhsia bora na hivyo mimi hujaribu kuwa mtu mzuri,” alisema wakati akihojiwa na gazeti la Independent mwaka jana. Mchezaji huyo Mwafrika anasema yeye husali mara tano kwa siku, havuti sigara wala hanywi pombe.
Demba Ba ambaye asa ni raia wa Ufaransa ana asili ya Senegal, nchi ya Magharibi mwa Afrika ambayo asilimia 90 ya watu wake ni Waislamu.
1405284

captcha