IQNA

Mwanasiasa wa Sweden Aivunjia Heshima Qur’ani Tukufu

10:36 - September 10, 2017
Habari ID: 3471165
TEHRAN (IQNA)-Mwanasiasa wa cha chama cha Democrats nchini Sweden amewakasirisha wengi kwa kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu.

Mattias Karlsson kiongozi wa bungeni wa chama cha Sweden Democrats (SD), ambacho kinapinga wahajiri kutoka nchi za Waislamu, hivi karibuni alitoa matamshi ya yenye chuki na kudai kuwa eti Qur’ani Tukufu ni sawa na kitabu cha ‘Mein Kampf’ (Mapambano Yangu) kilichoandikwa na Adolf Hitler mwaka 1925 akibainisha mitazamo yake ya kisiasa.

Karlsson alitoa matamshi hayo katika kikao cha ndani ya chama kilichokuwa kikijadili uchaguzi wa Septemba 17 wa Kanisa la Sweden ambapo chama cha SD kina wajumbe 1,000.

Katika hotuba yake katika ukumbi wa Gothenburg, Karlsson alisisitiza ulazima wa kuchukua tenda udhibiti wa Kanisa la Sweden ambalo alidai limezembea na kupelekea Uislamu kuenea Sweden.

Karlsson amelikosoa kanisa kwa kuwaalika Maimamu wa jamii za Waislamu katika makanisa na kuwaruhusu kusoma aya za Qur’ani Tukufu.

Karlsson ni muungaji mkono wa Rais Donald Trump wa Marekani ambaye aliwahi kusema kuwa Sweden inakabiliwa na mgogoro kutokana na kuwepo Wahajiri wengi Waislamu.

3639978

captcha