IQNA

Karakana ya kujenga milango ya Haram ya Imamyn Kadhimayn AS

Karakana ya kujenga milango Haram ya Imamyn Kadhimayn AS ilianza kazi zake mwaka 2011 katika mji wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran na hadi sasa milango 13 kati ya 16 inyohitajika imeshajengwa na kuanza kutumika huku milango mitatu iliyosalia ikitazamiwa kukamilika hivi karibuni.
Haram ya Imamyn Kadhimayn AS iko katika viungo vya mji wa Baghdad, Iraq na ni sehemu walimozikwa  Imam wa Saba wa Mashia, Imam Musa al-Kdhim AS na Imam wa Tisa wa Mashia, Imam Muhammad al-Jawad AS.
Milango hiyo imejengwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia mada kadhaa ikiwemo dhahabu ambapo wataalamu 40 wa kazi mbali mbali za sanaa ya ujenzi wamshiriki katika kazi hiyo. Milango hiyo inapokamilika inatumika katika eneo la Msikiti wa Safavi katika maziara hayo mawili ya Imamyan kadhimayn AS