Hayo yamedokezwa na mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma katika Jeshi la Iran, Hujjatul Islam Sayyed Akbar Mousavi wakati wa sherehe za kufungwa Mashindano ya Qur'ani ya Askari wa Jeshi la Nchi Kavi la Iran mjini Isfahan kati mwa Iran wiki hii.
Ameongeza kuwa tayari vituo 38 vya kuhifadhi Qur'ani vinakaribia kufunguliwa.
Sheikh Akbar Mousavi ameongeza kuwa, leo kuneshuhudiwa ongezeko kubwa la harakati za Qur'ani katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na majeshi mengine ya Iran.
Amesisitiza kuwa, utamaduni wa Qur'ani ndio nguzo kuu katika uwezo wa kujihami wa majeshi ya Iran.
Mashindano hayo ya Qur'ani yaliwashirikisha maafisa 300 wa Jeshi la Iran pamoja na familia zao.