IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Uwezo wa Hizbullah uliimarika baada ya vita vya siku 33

12:59 - July 14, 2019
Habari ID: 3472042
TEHRAN (IQNA) - Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza suala la kuimarika kwa nguvu na uwezo wa kujihami na kufanya mashambulizi wa wanamapambano katika kipindi cha miaka 13 iliyopita.

Aliyasehma hayo Ijumaa usiku mjini Beirut wakati alipofanya mahojiano na televisheni ya al Manar kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 13 tangu baada ya vita vya siku 33 huko Lebanon na kubainisha taathira za vita hivyo kwa Lebanon na eneo zima la Mashariki ya Kati (Asia Magharibi).
Mwaka 2006, Israel ilishindwa vibaya katika vita vya siku 33 baada ya kushindwa na wanamapambano wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, na kuilazimisha Tel Aviv kuomba usitishaji vita na kukubali masharti ya harakati hiyo.
Lebanon inajitegemea katika usalama
Kilichodhihiri huko Lebanon katika miaka 13 iliyopita ni kuimarika zaidi hali ya usalama ndani ya nchi hiyo kutokana na uwepo harakati ya Hizbullah. Hii ni katika hali ambayo usalama wa baadhi ya nchi za Kiarabu hususan Saudi Arabia unategemea himaya ya Marekani na ndio maana nchi hizo hulazimika kuipatia Marekani kitita kikubwa cha fedha. Lebanon kwa upande wake haihitaji dola lolote ajinabi kudhamini usalama wake kutokana na kuwepo Hizbullah nchini humo. Kuhusiana na suala hilo, Katibu Mkuu wa harakati hiyo amesema kuwa: Ni miaka 13 sasa ambapo Lebanon ipo katika hali ya usalama na hali inatokana na jitihada za Walebanoni wenyewe. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa kama Hizbullah isingekuwepo Lebabon isingekuwa na moja kati ya nguzi zake muhimu. Ukweli wa mambo ni kuwa, amani inayoshuhudiwa huko Lebanon inatokana na kuwepo harakati ya Hizbullah na kuimarika uwezo na nguvu ya harakati hiyo. Wakati huo huo sababu kuu ya uadui wa Marekani dhidi ya Hizbullah ni kwamba harakakti hiyo inazuia utegemezi wa Lebanon kwa Washington, na katika upande mwingine, kuzidi kuimarika na kupata nguvu Hizbullah siku baada ya siku kumeitia wasiwasi Israel; jambo ambalo ni tishio kwa utawala huo ghasibu.
Marekani imekiri kuhusu uwezo wa Hizbullah
Marekani pia imekiri kwamba Hizbullah imeimarika na kupata nguvu kubwa aidi. Ni kwa kutilia maanani hali hii, ndio maana Marekani ikaamua kuiweka Hizbullah katika orodha ya vikwazo vyake, na vilevile wabunge wenye mfungamano na harakati hiyo ndani ya Bunge la Lebanon wamejumuishwa katika orodha hiyo ya vikwazo vya Washington.
Kuhusiana na suala hilo, Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa "Harakati ya Hizbullah ipo katika faharasa ya vikwazo vya Marekani tangu muongo wa 80, hata hivyo muqawama umeimarika zaidi licha ya vikwazo vyote hivyo. Suala jipya ni kuwa wawakilishi wa Hizbullah katika Bunge la Lebanon wamewekwa katika orodha ya vikwazo vya Marekani na hiyo ni dharau na kulivunjia heshima Bunge na Serikali ya Lebanon."
Mlingano wa nguvu
Nukta ya tatu iliyoashiriwa na Sayyid Hassan Nasrullah katika hotuba yake ni kuhusu mlingano wa nguvu katika eneo la Mashariki ya Kati kwa maslahi ya mhimili wa muqawama. Leo hii muqawama dhidi ya maghasibu Wazayuni umepata nguvu katika eneo la Asia magharibi kiasi kwamba, hakuna dola linaloweza kuthubutu kufanya mashambulizi dhidi ya pande za muqawama huo. Katika uwanja huo, Sayyid Hassan Nasrullah ameashiria nukta kadhaa kuhusu suala hilo. Nukta ya kwanza ni namna muqawama ulivyoimarika zaidi katika miaka 13 iliyopita jambo ambalo Israel pia imelikiri. Sayyid nasrullah anasema: Nukta ya pili ni kuwa, mwaka 2006 nilisema nikiwa huko Binti Jubeil kwamba Israel ni dhaifu zaidi kuliko hata nyumba ya buibui na imani yetu kuhusiana na suala hilo imeimarika zaidi.
Muamala wa karne
Nukta nyingine muhimu iliyoiashiriw naa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ni sisitizo lake kuhusu kushindwa mpango eti wa "Muamala wa Karne." Nasrullah ameashiria jinsi Jared Kushner, Mshauri wa Rais Donald Trump wa Marekani katika masuala ya Mashariki ya Kati alivyokiri kwamba kikao cha Manama cha kuzindua mpango huo kimefeli na kueleza kuwa: "Tunaamini kwamba Muamala wa Karne utagonga mwamba. Kamwe hamtampata Mpalestina yoyote au Muislamu au Mkristo ambaye atakubaliana na suala la kuipatia Israel matukufu ya Kiislamu na Kikristo; na huu ndio udhaiui mkubwa zaidi wa mpango wa eti Muamala huo wa Karne."
Marekani itapata hasara katika vita na Iran
Mvutano baina ya Marekani na Iran ni suala jingine lililoashiriwa kwenye hotuba ya Sayyid Hassan Nasrullah alipofanyiwa mahojiano hayo.
Hali ya mivutano imeshuhudiwa kuongezeka katika miezi ya karibuni kati ya Iran na Marekani na waitifaki wake. Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon anaamini kuwa, mivutano hiyo haitasababisha vita kwa sababu kamwe Iran haitaanzisha vita na Marekani na Washington pia inajua vyyema kuwa vita kati yake na Iran vitakuwa na gharama kubwa. Kwa mtazamo wa Sayyid Hassan Nasrullah ni kuwa, vita dhidi ya Iran vitalikumba pia katika eneo zima la mashariki ya kati. Kwa mtazamo wa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Marekani ina wasiwasi mkubwa aidi kuhusiana na usalama wa Israel kuliko chochote kile na inauhesabu usalama wa waitifaki wake wa Kiarabu kuwa wenye umuhimu wa kiwango cha chini kwa Washington ikilinganishwa na usalama wa utawala ghasibu wa Israel.

3473035

captcha