IQNA

Wanawake Saudia

Wanawake waanza kuendesha treni ya Makka-Madina nchini Saudi Arabia

20:20 - January 03, 2023
Habari ID: 3476350
TEHRAN (IQNA) – Wanawake wameruhusiwa kuendesha treni zinazosafiri kati ya miji mitakatifu ya Makka na Madina nchini Saudi Arabia.

Shirika la Reli la Saudi limetoa video ya wanawake wanaoendesha treni inayojulikana kama Treni ya Makka-Madina Haramain ambapo wanaonekana wakiwa wanapokea mafunzo wakiwa wamekaa kwenye kiti cha udereva.

Wanawake hao Wasaudi wanaonekana wakiwa na shughuli nyingi wakitekeleza majukumu yao kwenye treni katika klipu ya video ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Shirika la Reli la Saudi lilitangaza kuwa wanawake 31 wenye asili ya nchi hiyo wamemaliza mafunzo ya kuendesha treni za mwendo kasi.

Treni ya mwendo kasi ya Makka-Madina Haramain ni mojawapo ya treni zenye kasi zaidi duniani.

Mwanamke wa Saudi Sara Al Shehri alisema, "Mimi na wafanyakazi wenzangu tumekuwa wa kwanza kuwa na heshima ya kuendesha treni ya mwendo wa kasi katika Mashariki ya Kati, ambayo ninajivunia."

Noorah Hisham, mwanamke mwingine wa Saudi aliyemaliza mafunzo hayo, anasema kuwa ni kazi yenye majukumu makubwa. Usalama wa wale wanaokuja nchini kwa ajili ya Hija, Umrah, na Ziarat ni jukumu la dereva wa Haramain Express.

Dereva wa kike wa Saudia Shajin al-Mursi alisema kuwa ni jambo la fahari kubwa kuwa sehemu ya kundi la kwanza kupata mafunzo ya udereva wa treni.

3481916

captcha