Ee Mwenyezi Mungu! Nipe nguvu za kuniwezesha kufuata amri zako, Unionjeshe katika mwezi huu Utamu ya kukutaja (kila wakati), Uniwezeshe kutekeleza wajibu wa kukushukuru neema zako na Unihafidhi katika mwezi huu katika ulinzi wako wa sitara yako Ewe Mwenye kuona zaidi ya waoni.