IQNA

Qarii Al-Toukhi akisoma baadhi ya aya za Surah Al-Ma'idah

23:17 - August 06, 2020
Habari ID: 3473041
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Muhammad al-Toukhi alikuwa qarii mashuhuri wa Qur'ani Tukufu kutoka Misri.

Al-Toukhi alizaliwa katika kijiji kimoja jimboni Qalyubiyya kaskazini mashariki mwa kaskazini mashariki mwa Misri na alianza kupenda kusoma Qur'ani akiwa bado mtoto.

Anasema baba yake alipelekea Madrassah ya Qur'ani akiwa mdogo na kwanza alihifadhi Qur'ani kabla ya kuanza kujifunza qiraa.

Al-Toukhi anasema kwanza aliwaiga maqarii muhimu kama vile   Abdul Basit Abdul Samad, Mustafa Ismail, Mohamed Sidiq Minshawi na Mahmodu Ali al-Bana.

Sheikh Al- Toukhi ametembea katika nchi nyingi duniani na anasema alitembelea madrassah za Qur'ani nchini Tanzania ambazo zinafunza qiraa yenye kuiga usomaji wa Wamisri. Sheikh Al Toukhi alifariki Machi 6, 2009 akiwa na umri wa miaka 87.

Qiraa iliyopo hapa chini ni ya Sheikh Al-Toukhi akisoma baadhi ya aya za  Surah Al-Ma'idah.

 

3914674

captcha