IQNA

Kiongozi wa Waislamu ahujumiwa Minnesota Marekani, CAIR yataka uchunguzi

22:27 - August 09, 2020
Habari ID: 3473050
TEHRAN (IQNA) – Polisi katika jimbo la Minnesota Marekani wanawasaka vijana wawili ambao walimpiga na kumuumiza kiongozi wa Waislamu katika eneo hilo. Vijana hao wawili wanakisiwa kuwa na umri wa miaka 20 hivi na mmoja ni mzungu huku mwingine akiwa na asili ya Afrika.

Tukio hilo lilijiri saa nne usiku Alhamisi karibu na msikiti wa Darul Farooq. Kiongozi huyo wa Waislamu aliyelengwa ametajwa kuwa Sheikh Mohamed Mukhtar mwenye umri wa miaka 50. Mkurugenzi wa Msikiti wa Darul Farooq amesema Waislamu daima wanaishi katika hofu ya kuhujumiwa.

Kufuatia tukio hilo, Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani, CAIR, Tawi la Minnesota limetaka wakuu wa jimbo hilo wafanya uchunguzi kamili kuhusu hujuma hiyo.

Tukio hilo limejiri kairbuni miaka mitatu baada ya msikiti huo kuhujumiwa na kuharibiwa vibaya.

3472219

Habari zinazohusiana
captcha