Taarifa ya wizara hiyo imesema misikiti hiyo ni asilimia 24 ya misikiti yote katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika
Katika duru ya kwanza, misikiti itaruhusiwa kuwa wazi kwa waumini dakika 15 kabla ya swala za kila siku na kufungwa dakika 10 baada ya swala.
Aidha Wizara ya Wakfu ya Algeria inasisitiza kuhusu ulazima wa kuzingatia kanuni zote za kiafya zinazotekelezwa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.
Siku ya Jumamosi Algeria ilitangaza itaondoa baadhi ya sheria zilizokuwa zimewekwa ili kuzuia kuenea corona ikiwa ni pamoja na kuondoa kafyu wakati wa usiku, kuondoa marufuku ya safari na kuruhusu misikiti mikubwa kufunguliwa.
Hadi sasa watu 35,160 wameambukizwa corona Algeria huku wengine 1,302 wakiripotiwa kufariki.