IQNA

Misikiti 4,000 kufunguliwa tena Algeria

15:33 - August 10, 2020
Habari ID: 3473053
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu ya Algeria imesema misikiti 4,000 nchini humo iko tayari kufunguliwa baada ya kutimiza masharti yanayotakiwa katika kipindi hiki cha janga la COVID-19 au corona.

Taarifa ya wizara hiyo imesema misikiti hiyo ni asilimia 24 ya misikiti yote katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika

Katika duru ya kwanza, misikiti itaruhusiwa kuwa wazi kwa waumini dakika 15 kabla ya swala za kila siku na kufungwa dakika 10 baada ya swala.

Aidha Wizara ya Wakfu ya Algeria inasisitiza kuhusu ulazima wa kuzingatia kanuni zote za kiafya  zinazotekelezwa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Siku ya Jumamosi Algeria ilitangaza itaondoa baadhi ya sheria zilizokuwa zimewekwa ili kuzuia kuenea corona ikiwa ni pamoja na kuondoa kafyu wakati wa usiku, kuondoa marufuku ya safari na kuruhusu misikiti mikubwa kufunguliwa.  

Hadi sasa watu 35,160 wameambukizwa corona Algeria huku wengine 1,302 wakiripotiwa kufariki.

3915728

captcha