IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Wapalestina wamepasi vizuri mtihani, adui mwenye sifa za mbwa mwitu ameelewa hawezi kufanya lolote

9:26 - May 22, 2021
Habari ID: 3473934
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu na kuupongeza muqawama wa Palestina kwa ushindi wake katika vita vya siku 12 kati yake na utawala wa Kizayuni.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei sambamba na kutuma pongezi zake kwa vijana mashujaa na wenye ghera, makundi ya muqawama na Ghaza ya mashujaa na iliyosimama imara, amesema kuwa, tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mwenye nguvu kwa kuwapa ushindi na heshima wanajihadi wa Palestina na tunamuomba azipe utulivu nyoyo za familia za mashahidi, awamiminie rehema Zake mashahidi na awape afueni kamili wote waliojeruhiwa, kama ambavyo tunatoa pongezi kwa mashujaa hao kwa kuushinda utawala wa Kizayuni wa watenda jinai.

Amesema, taifa la Palestina limepasi vizuri mtihani wa siku hizi chache na kuongeza kuwa, adui mwenye sifa za mbwa mwitu ameelewa vizuri sasa kwamba hawezi kufanya lolote mbele ya mapambano ya kauli moja ya Wapalestina.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, ushirikiano mzuri ulionekana baina ya Quds na Ukingo wa Magharibi na ardhi nyingine za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu tangu mwaka 1948 na Ghaza na kambi za wakimbizi wa Palestina; umewaonesha Wapalestina njia sahihi ya kufuata. Amesema, katika siku hizi 12, utawala katili wa Kizayuni umetenda jinai kubwa hasa huko Ghaza na umethibitisha kivitendo kuwa uko tayari kufanya vitendo viovu mno na vya kiwendawazimu kupindukia kutokana na kushindwa kukabiiana na mapambano ya kauli moja ya Palestina.

Hata hivyo kwa jinai zake hizo zisizo na kifani, utawala wa Kizayuni umezikasirisha fikra za wanadamu wote duniani. Jinai hizo kubwa zimepelekea kuzidi kuchukiwa na dunia madola ya kibeberu ya Magharibi hasa Marekani kwa kuunga mkono jinai za Wazayuni. (Wazayuni wamekumbwa na wakati mgumu, kwani) kuendelea na jinai au kuomba kwao kusimamishwa vita, kote kuwili kuna maana ya kushindwa utawala wa Kizayuni ambao hatimaye umelazimika kukiri kushindwa. 

3972855

captcha