IQNA

Iran yataraji kutuma Mahujaji 2,000 mwaka huu

17:56 - June 01, 2021
Habari ID: 3473970
TEHRAN (IQNA) – Afisa mwandamizi wa Hilali Nyekundi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema yamkini Iran ikatuma mahujaji wasiozidi 2,000 kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu nchini Saudi Arabia.

Ali Marashi amesema serikali ya Saudia imesema itapokea Mahujaji 60,000 kutoka nje ya ufalme huo mwaka huu. Ameongeza kuwa, mahujaji wengine 15,000 watatoka ndani ya Saudi Arabia.

Marashi amesema kwa kuzingatia idadi ya raia wa Iran ambao walikuwa wanaruhusiwa kuhuji miaka iliyopota, mwaka huu Wairani ambao kisheria wanatakuwa Kuhiji ni 1,500 tu lakini kutokana na kuboreka uhusiano wa Iran na Saudia, idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka na kufika 2,000.

Mwaka 2019, karibu Wairani 85,000 walijiunga na Waislamu karibuni milioni 2.5 kutekeleza Ibada ya Hija. Mwaka jana kutokana na janga la corona ni Waislamu wasiozidi karibu 1000 walioweza kutekeleza ibada ya Hija na wote walikuwa ni wakazi wa Saudia.

Aidha amesema Mahujaji wote wanatakiwa kupata chanjo ya COVID-19 na wawe na umri wa baina ya miaka 18-60.

Ufalme wa Saudi Arabia umesema Waislamu wanaokusudia kutekeleza ibada ya Umrah katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ni sharti kwanza wapate chanjo ya COVID-19 au corona.

Oktoba mwaka jana Saudi Arabia ilifungua tena milango ya Msikiti mtakatifu wa Makka kwa ajili ya Swala baada ya kufungwa kwa kipindi cha miezi 7 kutokana na hofu ya maambukizi ya corona. 
Mwaka jana pia Saudia Arabia ilizuia ibada ya Hija kwa wahujaji wote kutoka nje ya nchi hiyo na kuruhusu watu elfu 10 tu wa ndani kutekeleza ibada hiyo muhimu ya Kiislamu. 

Maelfu ya Wasaudia wamepoteza maisha hadi sasa kutokana na ugonjwa wa Covid-19.  

3974809

captcha