IQNA

Rais Hassan Rouhani

Fikra za Imam Khomeini (MA) kuhusiana na Mapindizi ya Kiislamu ziliegemea kwa wananchi

18:02 - June 02, 2021
Habari ID: 3473971
TEHRAN (IQNA)- Fikra za Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu Amrehemu- kuhusiana na harakati na Mapindizi ya Kiislamu ziliegemea kwa wananchi, amesema Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Rais Hassan Rouhani ambaye alikuwa akizungumza katika baraza la mawaziri leo Jumatano kabla ya maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya kuaga dunia Imam Ruhullah Khomeini amezitaja siku za tarehe 13, 14 na 15 mwezi Khordad (mwaka wa Hijria Shamsia) kuwa ni siku zenye umuhimu mkubwa katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.

Rais Rouhani ameongeza kuwa, masanduku ya kupigia kura ni miongoni mwa matokeo na matunda muhimu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yaliyouondoa madarakani utawala wa kifalme na kidhalimu. Aidha amesema njia iliyoainishwa na hayati Imam Ruhullah Khomeini kwa ajili ya kuongoza nchi ni chaguzi na kura za wananchi, na kwamba kaulimbiu kuu ya mwasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ilikuwa "kura za wananchi ndiyo mizani". 

Rais Rouhani amesema kuwa, Imam Khomeini aliamini kwamba, wananchi wanapaswa kuwa na nafasi muhimu katika madaraka na uendeshaji wa nchi. 

Amesisitiza kuwa Kiongozi wa sasa wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei pia amekuwa akitilia mkazo umuhimu wa kushiriki kwa wingi wananchi katika chaguzi mbalimbali na kwa msingi njia hiyo ya Imam bado inaendelea. 

Amezungumzia pia vikwao na njama za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi chote cha baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema: Ujumbe tulioipatia dunia, rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na viongozi wa nchi nyingine ni kuzindua miradi kabambe ya kiuchumi iliyovunja migongo ya mabeberu hao. 

/3975196

captcha