IQNA

ISWAP: Kinara wa Boko Haram Abubakar Shekau amejiua

18:39 - June 07, 2021
Habari ID: 3473987
TEHRAN (IQNA) – Kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) Afrika Magharibi, ISWAP, limethibitisha katika ujumbe wa sauti kwamba kinara wa kundi la kigaidi la Boko Haram la Nigeria, Abubakar Shekau amejiua na kuelekea jongomeo.

Uthibitisho huu umetolewa wiki mbili baada ya ripoti kuibuka kwamba alikuwa  kinara huyo wa Boko Haram amefariki.

 Shirika la habari la AFP limesema lilipokea mkanda wa sauti inayofanana na kiongozi wa ISWAP, Abu Musab Al-Barnawi, akizungumza kwa lugha ya Kanuri ya Nigeria, ambapo alisema eti Shekau alipendelea 'kujifedhehesha katika maisha ya akhera kuliko kufedheheshwa hapa duniani', na kuelezea kwamba alijiua mara moja kwa kujiripua. Sauti hiyo ilikabidhiwa kwa AFP na chanzo kilichotuma ujumbe wa awali kutoka kundi hilo. Kundi la kigaidi la Boko Haram bado halijatoa tamko rasmi kuhusu kifo cha kinara wake huyo , ambaye aliendesha uasi wa zaidi ya muongo mmoja kaskazini-mashariki mwa Nigeria, huku jeshi la Nigeria likisema linachunguza madai hayo.

Msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedia Jenerali Mohammed Yerima amesema kwamba jeshi lilikuwa linachunguza kile kilichotokea, lakini halitatoa taarifa hadi lipate uthibitisho rasmi. Shekau aliwahi kurpotiwa kufa mara kadhaa miaka ya nyuma, lakini akijitokeza tena.

Baada ya kuchukua uongozi wa kundi la  Kiwahhabi la Boko Haram mwanzilishi wake alipofariki katika kizuizi cha polisi mwaka 2009, Shekau aliongoza mabadiliko yake kutoka kwa kundi la kawaida lenye misimamo mikali hadi kuwa kundi la ugaidi wa kinyama ambao umeenea kaskazini-mashariki mwa Nigeria na nchi jirani.

Tangu alipochukua uongozi wa Boko Haram, zaidi ya watu 30,000 wameuawa na wengine zaidi ya milioni mbili kufurushwa makwao hasa eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria.

3474908

 

captcha