Hii ni mara ya kwanza kwa Sala ya Idi kusaliwa hapo baada ya kusitishwa kwa miaka miwili kutokana na maambukizi ya corona ambayo sasa yamepungua sana nchini Iraq.
Sala ya Idul Fitr imesalishwa na Sheikh Murtadha Qazwini ambaye ametoa wito kwa waumini kumshukuru Allah SWT kwa kujaalia Haram Takatifu za Ahul Bayt wa Mtume Muhammad SAW katika miji ya Iraq.
Aidha ameipongeza serikali ya Iraq kwa kuimarisha usalama nchini humo. Sala ya Idi imesaliwa mara kadhaa katika eneo hilo jana kutokana na idadi kubwa ya waumini walioshiriki.
Maelfu ya Waislamu wa Iraq jana walishiriki katika Sala ya Idul Fitr baada ya kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Baadhi ya mataifa ya Kiislamu kama Saudi Arabia, Uturuki, Misri, Qatar, Kuwait na Palestina yaliadhimisha sikukuu ya Idul Fitr jana huku mataifa mengine ya Kiislamu kama Iran, Tanzania, Pakistan na Iraq yakisherehekea sikukuu hiyo Jumanne ya jana.