IQNA

Wanamichezo Waislamu

Paul Pogba ajiunga na kampuni ya kifedha ya Kiislamu ‘Balozi wa Chapa’

22:38 - June 11, 2022
Habari ID: 3475365
TEHRAN (IQNA)-Mwanasoka Mfaransa Muislamu alijiunga na Wahed Inc., kampuni ya kimataifa ya Kifedha ya Kiislamu, kama mwekezaji na ‘Balozi wa Chapa’.

Paul Pogba, bingwa wa Kombe la Dunia la 2018, alijiunga na mabalozi wa sasa wa chapa ambao ni bingwa wa UFC Khabib Nurmagomedov, na timu yake ya wapiganaji karate.

Poga ambaye alianza maisha yake ya soka akiwa na umri wa miaka sita ni maarufu kama mchezaji katika klabu ya  Manchester United ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na timu ya taifa ya Ufaransa ambapo hucheza kama kiungo wa kati.

Afisa Mkuu Mtendaji Wahed, Junaid Wahedna na Pogba walikutana mnamo Septemba 2021 kuweka mkakati wa kuhimiza uwekezaji wenye maadili na kwa bei nafuu, ambapo Poga aliafiki kuwa ‘Balozi wa Chapa’ wa shirika hilo la kifedha la Kiislamu, kampuni hiyo ilisema.

Pogba alisema: "Nilijua nilitaka kuwa sehemu yake, kwa muda mrefu tukiinukia, hatukuweza kupata njia salama ya kusimamia na kukuza fedha zetu."

Mfaransa huyo anatumai kwamba ushirikiano wake na Wahed utasaidia kuwaonyesha vijana kwamba kuna njia za kuanza kuwekeza kwa njia sahihi na "ni busara kuanza kufikiria malengo ya muda mrefu ya kifedha mapema maishani."

Wahedna alisema “Pogba ni kiongozi anayefanya vizuri katika tasnia yake, ambayo inaendana na maono na dhamira ya kile tunachojaribu kufikia,” na kuongeza, “Tunafuraha kubwa kumkaribisha kama balozi wetu mpya wa chapa tunapoendelea kutafakari upya mfumo  bora wa kifedha."

Wahed imepata uungaji mkono wa wawekezaji kwa kasi tangu kuanzishwa kwake na ina zaidi ya wateja 300,000 duniani kote katika mashirika yake yote.

3479259

captcha