IQNA

Qarii wa Qur'ani

Qiraa ya kipekee ya Surah Maryam ya Sheikh Mustafa Ismail

14:02 - June 18, 2022
Habari ID: 3475390
TEHRAN (IQNA)- Klipu hii hapa chini inaonyesha qarii mtajika wa Qur'ani Tukufu kutoka Misri Mustafa Ismail akisoma aya yza 30-36 za Qur'ani Tukufu.

Qiraa hii inasambazwa kwa mnasaba kwa mnasaba wa Juni 17 ambayo ni siku ya kukumbuka kuzaliwa qarii huyu mashuhuri wa Misri.

Tarjuma ya aya hizi ni kama ifuatavyo:

Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai. Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.

Sheikh Mustafa Ismail aliyezaliwa Juni 17,1905 katika eneola Tanta jimboni Gharibia nchini Misri na alikuwa miongoni mwa wasomaji mashuhuri zaidi wa Qur'ani Tukufu nchini Misri.

Alikuwa na mtindo maalumu wa qiraa na aliweza kuwavutia wengi kutokana na usomaji wake. Qarii mashuhuri wa Misri katika zama hizi Sheikh Ahmed Ahmed Noaina amesema, "Mustafa Ismail alikuwa na mbinu kadhaa za qiraa na hadi sasa hakuna mtu aliyweza kuja na mbinu mpya baada yake.

Alianza kujifunza Qur'ani Tukufu na misingi ya Tajwidi kutoka kwa Sheikh Idris Fakhir. Alizana qiraa ya Qur'ani mbele ya hadhara kubwa akiwa na umri wa miaka 4 katika Msikiti wa Atif eneo la Tanta ambapo sauti yake iliwavutia wengi. Aliendeleza kipaji chake kwa kuelekea Cairo ambapo alikuwa mwanafunzi wa Qarii Sheikh Muhammad Rafa'at. Alipata umashuhuri na akaanza kualikwa katika nchi mbali mbali kusoma Qur'ani Tukufu kama vile Iraq, Indonesia, Saudi Arabia, Pakistan, Ujerumani, Palestina, Uingereza na Ufaransa.  Aidha alitunukiwa tunzo kadhaa kitaifa na kimataifa kutokana na umahiri wa qiraa yake ya Qur'ani Tukufu. Hatimaye Sheikh Mustafa Ismail aliaga dunia na kurejea kwa Mola wake mnamo Disemba 26, 1978.

4064785

 

captcha