IQNA

Bidhaa Halal

Mswada wa kupiga marufuku uchinjaji 'Halal' wafutwa Ubelgiji

10:51 - June 19, 2022
Habari ID: 3475395
TEHRAN (IQNA) – Waliokuwa wakitaka marufuku uchinjaji nyama kwa msingi wa dini za Kiislamu na Kiyahudi nchini Ubelgiji wamepata pigo baada ya mswada wao kushindwa katika mji mkuu wa Brussels.

Brussels ni makao makuu ya Umoja wa Ulaya na eneo pekee la Ubelgiji ambako uchinjaji kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu au 'Halal' na uchinjaji kwa mujibu wa mafundishi ya Kiyahudi  au 'Kosher' bado unaruhusiwa

Kura ya Ijumaa katika bunge la Mkoa wa Brussels-Eneo la Capital - moja ya majimbo matatu ambayo yanajumuisha ufalme wa shirikisho wa Ubelgiji - ilikuwa juu ya kufuta mswada unaopendekeza kupigwa marufuku uchinjaji wa mifugo kwa mujibu wa misingi ya 'Halal' na 'Kosher'. Mswada huo uliwasilishwa na vyama vya kiliberali na vinavyozingatia mazingira.

Brussels, jiji ambalo ni  makao makuu ya idadi kubwa ya taasisi za Umoja wa Ulaya, na hivyo mara nyingi hutazamwa kama nembo ya umoja huo. Kote katika Ulaya Magharibi, wanasiasa wenye mitazamo ya kiliberali wamekuwa wakioneza kampeni ya kupigwa marufuku uchinjaji 'Halal' na 'Kosher'.

Vyama vingi vinavyoonekana kupinga Uislamu, na wakati mwingine pia Uyahudi, vinaunga mkono kupiga marufuku uchinjaji 'Halal' na 'Kosher' kwa sababu wanaona uchinjaji huo ishara za ushawishi wa kigeni. Vyama hivyo pia vinaunga  mkono kupiga marufuku tohara wavulana, ambayo Waislamu na Wayahudi wameamriwa kufanya.

3479348

captcha