IQNA

Soko la 'Halal'

Kampuni za Chakula za Korea Kusini Zinavutiwa na Kugusa Soko la Halal Ulimwenguni

21:07 - June 22, 2022
Habari ID: 3475411
TEHRAN (IQNA) – Makampuni ya chakula ya Korea Kusini yanatilia maanani soko la 'Halal' katika nchi mbalimbali.

Halal ina maana ya "vitu vinavyoruhusiwa" katika Kiarabu, na inahusu bidhaa kama chakula, vipodozi n.k pamoja na huduma ambazo zimetayarishwa kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu.

Bidhaa za chakula ambazo hazina kilevi na zilizotengenezwa kwa nyama kama vile ng'ombe, kondoo na mbuzi zilizochinjwa kwa mujibu wa taratibu za Kiislamu ndizo pekee zinaweza kupata kibali cha  'Halal'. Bila kibali  cha 'Halal', haiwezekani kuuza chakula katika nchi za Kiislamu au katika maduka maalumu ya bidhaa 'Halal' duniani.

Baada ya janga la COVID-19, chakula chenye nembo ya 'Halal' kimekuwa maarufu kama chakula safai hata miongoni mwa wasiokuwa Waislamu. Makampuni ya chakula cha ndani ya Korea Kusini yanapanua kikamilifu biashara yao ya kimataifa kwa kuingia katika soko la 'Halal', ambalo lina uwezo mkubwa wa ukuaji.

Kwa mujibu wa Shirika la Korea Kusini la Ustawishaji Bishara na Uwekezaiji (KOTRA), soko la Halal duniani, ikiwa ni pamoja na chakula, vinywaji, mavazi, dawa na vipodozi, inakadiriwa kuwa dola trilioni 4.5 mwaka 2020. Miongoni mwao, soko la chakula 'Halal' lilikua na kufikia trilioni 1.9 mwaka jana.

Soko la halal linachangia asilimia 26 ya soko la chakula duniani na linakua kwa asilimia 10-15 kila mwaka. Kwa kuzingatia kwamba wastani wa ukuaji wa kila mwaka wa masoko mengine ya chakula ni asilimia 1-2, soko la chakula 'Halal' linakua kwa kasi.

Kampuni za chakula za Kikorea pia zinalenga soko la 'Halal'

Kwa mfano Shirika la CJ CheilJedang imeendelea kupanua biashara yake ya chakula cha 'Halal' tangu ilipopata cheti cha 'Halal' kwa bidhaa zake 30 za chakula kutoka Idara ya Ustawi wa Kiislamu ya Malaysia (JAKIM) mwaka 2011.

Pia imepata cheti cha  'Halal' kutoka Majlis Ulamaa Indonesia maarufu kama na Wakfu wa Waislam wa Korea (KMF) katika kipindi cha miaka 10 iliyopita na inasambaza bidhaa za halali kwa nchi 110, ikiwa ni pamoja na Malaysia, Indonesia, Mashariki ya Kati, Thailand na Singapore.

Shirika la Daesang Food nalo limepata cheti cha 'Halal' kwa takriban bidhaa 50 tangu ianze kuuza nje vyakula vya 'Halal' mnamo Februari 2011.

3479419

captcha