IQNA

Jinai za Israel

Umoja wa Mataifa wathibitisha Shireen Abu Akleh aliuawa na wanajeshi wa utawala wa Israel

18:33 - June 24, 2022
Habari ID: 3475420
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa umesema uchunguzi umebaini kuwa , Shireen Abu Akleh, mwandishihabari Mpalestina wa televisheni ya al-Jazeera ya Qatar aliuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ravina Shamdasani, Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) amesema: Taarifa zote tulizokusanya zinalandana, na zinaonesha kuwa risasi zilizomuua Abu Akleh na kujeruhi mwenzake Ali Sammoudi zilifyatuliwa na vikosi vya usalama vya Israel.

Shamdasani amesema hayo leo Ijumaa katika kikao na waandishi wa habari mjini Geneva na kueleza bayana kuwa, hakuna ushahidi wowote wa kuonesha kuwa risasi hizo zilifyatuliwa ovyo na wapiganaji wa Palestina.

Amefafanua kwa kusema kuwa, taarifa zilizokusanywa na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, hakukuweko na raia yeyote wa Palestina aliyejizatiti kwa silaha karibu na eneo alikouawa mwanahabari Abu Akleh.

Hii ni katika hali ambayo, uchunguzi mpya wa gazeti la Marekani la New York Times umethibitisha pia kuwa, risasi iliyomuua Shireen Abu Akleh, ilifyatuliwa na mwanajeshi wa kikosi maalumu cha Israel.

Mapema mwezi uliopita wa Mei mwandishi wa habari ya televisheni ya Al Jazeera, Shireen Abu Akleh, 51, alipigwa risasi kichwani na kuuliwa kikatili na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakati akiwa kwenye kazi yake ya kuripoti uvamizi wa kijeshi wa jeshi la Israel katika kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Jenin.

3479436

captcha