IQNA

Utalii wa Kiislamu

Mawaziri wa Utalii wa OIC kufanya kukutana Baku

23:20 - June 26, 2022
Habari ID: 3475430
TEHRAN (IQNA) - Mawaziri wa Utalii wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wanatarajiwa kushiriki katika mkutano katika mji mkuu wa Jamhuri ya Azerbaijan, Baku kujadili maendeleo ya utalii katika nchi za Kiislamu.

Jiji la Baku litakuwa mwenyeji wa kikao hicho kuanzia tarehe 27 - 29 Juni 2022  na hicho kitakuwa ni kikao cha 11 cha Mkutano wa Kiislamu wa Mawaziri wa Utalii wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC)  ambacho kinafanyika chini ya mada "Nafasi ya Jamii  Maeneo katika Maendeleo ya Utalii".

Kikao hicho kitaangazia kuendeleza Mwongozo wa Maendeleo ya Utalii wa Kiislamu katika Nchi Wanachama wa OIC, kufuatia kupungua idadi ya watalii kimataifa, hasa kutokana na vikwazo vya usafiri na hatua nyingine zilizoenea za kudhibiti kuenea kwa virusi vya COVID-19.

Makadirio yanaonyesha kuwa, ikilinganishwa na 2019, nchi za OIC, kama kikundi, zilipokea watalii wachache wa kimataifa kwa asilimia 73 na kipato cha utalii kilipungua kwa asilimia 64 mnamo 2020.

Mkutano huo wa Mawaziri utapitia ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu utekelezaji wa Mwongozo wa OIC kuhusu Utalii, kutathmini maadhimisho ya kila mwaka ya Jiji la Utalii la OIC na kupendekeza programu za kuwezesha sherehe za mwaka mzima pamoja katika kuelekea kuchaguliwa washindi wapya wa tuzo za Mji wa Kitalii wa OIC katika mwaka wa  2023 na 2024.

Mawaziri wa Utalii wa OIC pia watakagua maendeleo ya baadhi ya miradi ya utalii ya nchi wanachama wa OIC, kutathmini maendeleo ya uandaaji wa Maonyesho ya Utalii ya OIC, kujadili changamoto zinazoikabili OIC kuhusu uandaaji wa mafanikio ya maonesho mbalimbali ya utalii, na kuendeleza pamoja mkakati wa maeonyesho yenye ufanisi.

3479462

captcha