IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Asilimia 50 ya Misikiti ya Uingereza imekabiliwa na hujuma za wenye chuki

15:51 - June 28, 2022
Habari ID: 3475436
TEHRAN (IQNA)- Uchunguzi mpya umebaini kuwa, karibu asilimia 50 ya misikiti yote nchini Uingereza imekumbana na hujuma za chuki dhidi ya Uislamu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Haya ni kwa mujibu wa utafiti wa kundi la kutetea Waislamu la Muslim Engagement and Development (MEND).

Ripoti hiyo iliyochunguza data kutoka misikiti zaidi ya 100 kote nchini Uingereza, pia iligundua kuwa asilimia 35 ya taasisi za Kiislamu zilikumbwa na shambulio la wenye chuki dhidi ya Uislamu angalau mara moja kwa mwaka.

Aina ya kawaida ya mashambulizi ni uharibifu, ikifuatiwa na wizi.

Mwenyekiti wa Msikiti wa Finsbury Park, ambao ulikumbwa na shambulio la kigaidi mwaka 2017, anasema hali sasa ni mbaya zaidi.

"Jamii yetu bado inahisi woga na vitisho, na wanatarajia kushambuliwa wakati wowote. Kilichotokea hakikuwa mara moja tu," anasema Mohammed Kozbar.

"Hali ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa miaka mitano iliyopita. Chuki dhidi ya Uislamu au Islampohobia inazidi kuongezeka, na hakuna anayeweza kukataa hilo," amebainisha.

Anasema kuwa Chuki dhidi ya Uislamu haijachukuliwa kwa uzito, na hadi hii itatokea - hakuna kitakachobadilika.

"Hatuna hata ufafanuzi wa maana hasa ya Islamophobia. Hatuna sheria au sheria za kulinda jamii bado. Kwa hivyo tunatumai serikali itachukua hatua," anasema Bw Kozbar.

Inakuja huku data mpya ya serikali ya Uingereza na Wales ikionyesha kuwa makosa yanayochochewa na kidini yapo juu sana.

Kulikuwa na jumla ya makossa ya jinai 76,884 yaliyochochewa na ubaguzi wa rangi na kidini yaliyorekodiwa mwaka wa 2021, ikiwa ni asilimia 15 zaidi  kutoka 66,742 mwaka wa 2020.

Kwa meneja wa eneo wa MEND, data hizi "ni dalili ya mwelekeo mpana wa chuki dhidi ya Uislamu."

Nayeen Haque alisema: "Tunaamini propaganda za chuki dhidi ya Uislamu zinazosambazwa katika jamii ndiyo sababu ya kuongezeka kwa mashambulizi ambayo tumeona katika jamii za Kiislamu."

Anasema kuna “kiwango cha wasiwasi” ambacho Waislamu wengi sasa wanakumbana nacho wanapozuru maeneo yao ya ibada.

"Lakini kwa kiasi kikubwa jamii  yetu ina uthabiti na tunataka kuonyesha ujumbe huu wa uthabiti na kwamba hii haitaathiri imani yetu," anaongeza Bw Haque.

Serikali ilizindua Mpango wa Usalama wa Maeneo ya Ibada (POW) kwa ajili ya maeneo ya England na Wales mwaka wa 2016, unaolenga kusaidia maeneo ya ibada ambayo yako katika hatari ya mashambulizi na uhalifu wa chuki.

3479474

captcha