IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mwanafunzi wa Misri ashika nafasi ya kwanza mashindano ya Qur'ani UAE

12:59 - June 29, 2022
Habari ID: 3475439
TEHRAN (IQNA)- Mwanafunzi wa taaluma ya tiba katika Chuo Kikuu cha Alezandria nchini Misri ameshika nafasi ya kwanza katika mashindano ya kuhifadhi Qur'ani ya wasichana katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Ayal Jamal Abdul Latif Bikr Muslim ameshika nafasi ya kwanza katika Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Zawadi ya Hessa bint Muhammad.

Akizungumza na Televisheni ya Misri, Ayah amesema alianza kuhifadhi Qur'ani Tukufu akiwa na umri wa miaka minne na amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani akiwa na umri wa miaka 14.

Anasema kuhifadhi Qur'ani Tukufu ni Baraka katika maisha yake kwani ndio sababu iliyompelekea kuweza kufanikiwa kuingia chuo kikuu kusoma tiba.

Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Taasisi ya Sultan bin Khalifa Al Nahyan kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu ya UAE kupitia idara yake ya Masuala ya Kiislamu na Wakfu.

Fatima Hassan al Ubaid wa Syria ameshika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Fatima Mahmoud Ali wa Somalia.

4067270

 

captcha