IQNA

Upinzani wa Israel

Majaji wa Algeria wakataa mwaliko wa Mkutano wa Tel Aviv

21:58 - September 18, 2022
Habari ID: 3475802
TEHRAN (IQNA) - Majaji wa Algeria wamesusia mkutano wa kimataifa huko Tel Aviv, huku wakibainisha sababu ya hatua hiyo ni upinzani wao kwa mkakati wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Katika taarifa, Baraza la Mahakimu  Algeria lilisema lilipokea mwaliko kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa ya Majaji kushiriki katika mkutano wake wa kila mwaka ambao mwaka huu unafanyika huko Tel Aviv mnamo Septemba 18-20.

Jumuiya hiyo ilisema iliijulisha rasmi jumuiya hiyo kuhusu uamuzi wake wa kususia mkutano huo.

"Uamuzi huo unaafikiana na msimamo rasmi na wa umma wa Algeria kuhusu kadhia ya Palestina na mshikamano na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina," ilisema taarifa hiyo.

Baraza la Mahakimu  Algeria ndilo chombo pekee cha uwakilishi wa majaji wa Algeria.

Algeria mara kadhaa ilitangaza kukataa kuhalalisha uhusiano na Israel hadi Tel Aviv itakapoacha kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina na kuanzishwa kwa taifa huru  la Palestina.

3480533

Kishikizo: algeria israel palestina
captcha