IQNA

Harakati ya Hizbullah

Nasrallah: Iran iko imara na matukio ya sasa hayawezi kuitikisa

20:19 - October 02, 2022
Habari ID: 3475867
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa ina nguvu na uthabiti kuliko wakati wowote ule, na kwamba taifa hili litavuka salama mtihani wa sasa kutokana na hekima ya viongozi wake.

Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon alisema hayo jana Jumamosi, ambapo ameashiria ghasia na machafuko ya hivi karibuni kote Iran yaliyosababishwa na kifo cha mwanamke wa Kiirani, Mahsa Amini aliyekuwa na umri wa miaka 22.

Sayyid Nasrallah amebainisha kuwa, licha ya makelele na propaganda za Wamagharibi, lakini Iran imeahidi kufanya uchunguzi wa kifo cha mwanamke huyo.

Amesema Wamagharibi wakiongozwa na Marekani wameendelea kuwachochea wananchi wa Iran kufanya ghasia na maandamano yenye uharibifu, ili kufuatilia malengo yake ya kishetani na kupanda mbegu za chuku miongoni mwa Wairani.

Watu 21 waliuawa huku wengine zaidi ya 20 wakijeruhiwa katika vitendo vya kigaidi vilivyofanyika juzi Ijumaa katika kivuli cha maandamano hayo, katika mji wa Zahedan, makao makuu ya mkoa wa Sistan na Baluchestan.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria undumakuwili wa Wamagharibi na kueleza kuwa, zaidi ya raia 50 waliuawa juzi Ijumaa katika shambulio la kigaidi lililolenga kituo cha kielimu cha Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Afghanistan, lakini hakuna Mmagharibi aliyepaza sauti kulaani unyama huo.

Nasrullah amesema maafisa wa serikali ya Marekani wanafahamu kuwa Iran ni nchi yenye nguvu na uwezo mkubwa na haiwezi kushindwi kwa kuitwika vita, na kwa msingi huo wameamua kuchochea machafuko hapa nchini.

Ameongeza kuwa, Wamagharibi wanajaribu kukuza fujo zinazoshuhudiwa hapa nchini, katika hali ambayo Jamhuri ya Kiislamu imepitia vipindi vizito zaidi huko nyuma.

3480693

Habari zinazohusiana
captcha