IQNA

Waislamu Uingereza

Ukumbi wa Royal Albert Hall wa London waandaa Futari

14:30 - April 09, 2023
Habari ID: 3476841
TEHRAN (IQNA) - Mamia walikusanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa kifahari wa Royal Albert Hall huko London kama sehemu ya futari ya wazi - tukio la kijamii wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Baada ya adhana Waislamu walifungua saumu ambayo ilifuatiwa na sala ya jamaa.

Akizungumza kabla ya Adhana, Balozi wa Uturuki nchini Uingereza Osman Koray Ertas, aligusia umuhimu wa Ramadhani katika kuimarisha uhusiano kati ya watu.

Alibainisha matetemeko makubwa ya ardhi ya Februari 6 nchini Uturuki na Syria na kusema waliohudhuria wana mshikamano na jamii ya Uturuki baada ya uharibifu huo.

Ertas aliwashukuru Waingereza kwa michango na kampeni za kuchangisha fedha kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi.

Jonathan Wilson, profesa katika Chuo Kikuu cha Regent's London, alisifu mikusanyiko ya wazi ya Futari na kusema mikusanyiko hiyo ni fursa nzuri sana ya kukutana na watu na kubadilishana uzoefu.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mradi wa Ramadan Tent, Dowshan Humzah, alisema miradi hiyo inawafanya watu wasiojuana kuwa marafiki.

Alibainisha matukio ya Futari ya miaka iliyopita na kuwashukuru wote ambao wamesaidia mradi huo. "Mradi wa Mahema ya Ramadhani haungekuwepo kama si watu wa kujitolea," alisema.

3483112

captcha