IQNA

Waislamu Uingereza

Uingereza: Kampeni ya Tembelea Msikiti Wangu 2023 Imezinduliwa

16:10 - September 05, 2023
Habari ID: 3477551
LONDON (IQNA) - Kampeni iliyopewa jina la "Tembelea Msikiti Wangu" ilizinduliwa Jumatatu kwa mwaka wake wa nane nchini Uingereza.

Imeandaliwa na Baraza la Waislamu la Uingereza (MCB), kampeni hiyo imeelezwa kuwa "tukio kubwa zaidi la siku ya wazi ya misikiti nchini Uingereza" na tovuti ya mwandaaji.

Zaidi ya misikiti 250 kote Uingereza iko tayari kufungua milango kwa majirani zao kwa nia ya kukuza uhusiano.

"Tembelea Msikiti Wangu 2023 utafanyika tarehe 23 na 24 Septemba. Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'imani, chakula na urafiki,' ambapo Misikiti na vituo vya Kiislamu vinavyoshiriki vitaleta pamoja jumuiya kwa ajili ya chai, ziara na mazungumzo," ilisema taarifa ya MCB.

Abdullah Quilliam Society, Msikiti wa kwanza wa Uingereza, na Msikiti Mkuu wa Cambridge, Msikiti wa kwanza wa Eco-friendly barani Ulaya, ni miongoni mwa misikiti inayoshiriki mwaka huu.

Katibu Mkuu wa MCB Zara Mohammed alibainisha wakati wa hafla ya uzinduzi kwamba misikiti sio tu ya sala.

“Misikiti ni zaidi ya sehemu ya kuswalia; ni vitovu vya jamii ambapo jumuiya mbalimbali za Kiislamu hukutana, taasisi ambazo zinaweza kutoa huduma mbalimbali muhimu kwa jumuiya za mitaa - kutoka kwa vilabu vya vijana na maeneo ya joto hadi benki za chakula, wazi kwa wale wote wanaohitaji," alisema.

Alitumai kwamba watu watapata "ufahamu wa kina" wa historia na kazi za misikiti ili "kuunda vifungo vya kudumu vya urafiki."

3485046

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uingereza waislamu
captcha