IQNA

Sayyid Hassan Nasrullah

Uchaguzi Syria ni thibitisho la kufeli njama za maadui

17:05 - June 07, 2014
Habari ID: 1414962
Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon, amesema kuwa kushiriki kwa wingi Wasyria katika uchaguzi wa rais nchini humo ni thibitisho kwa ulimwengu kwamba, mashinikizo ya Wamarekani na madola ya Magharibi na Kiarabu dhidi ya Syria, yameshindwa.

Aidha Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, uchaguzi huo ni tangazo la kisiasa na kitaifa la kufeli vita dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu. Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon ameyasema hayo Ijumaa katika maadhimisho ya kumuenzi Allamah Sheikh Mustwafaa Quswair, yaliyofanyika katika ukumbi wa Shahid Sayyid Muhammad Baqir Swadri katika shule ya Imam Mahdi AS mjini Bairut, Lebanon. Ameashiria vitisho vilivyotolewa kwa lengo la kuzuia uchaguzi wa rais nchini Syria na kusema kuwa, vitisho hivyo havikuwa na taathira yoyote, bali serikali ya Damascus ilisimama imara katika kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika katika tarehe iliyopangwa. Ameyahutubu, madola hayo ya Magharibi na waitifaki wao katika eneo la Mashariki ya Kati kwa kusema kuwa, yalitakiwa kuruhusu zoezi hilo kufanyika katika balozi za Syria ndani ya mataifa hayo ili waone kama ushiriki wa Wasyria ungekuwa mdogo au laa! Amesema Sayyid Hassan. Aidha amesema uchaguzi huo umedhihirisha ukweli huu kwamba, wananchi wa Syria ndio waamuzi na wenye kauli ya mwisho kuhusu mustakbali wa taifa lao na kwamba, vita vinavyoendelea nchini humo si kati ya serikali na wananchi, bali ni kati ya serikali na maadui wa taifa. Aidha amesema kuwa, ushiriki mkubwa wa wananchi umeonyesha kwamba raia wa nchi hiyo bado wana imani na serikali ya Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo. Amesema, yeyote anayetaka kutatuliwa mgogoro wa nchi hiyo kwa njia za kidiplomasia, hawezi kuupuuza uchaguzi wa rais nchini humo, hasa kwa kuzingatia kwamba uchaguzi huo umetoa ujumbe kwamba, utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa nchi hiyo, utaanza na kumalizika sambamba na Rais Bashar al-Assad kuwepo madarakani. Kwa upande mwingine amezungumzia propaganda zinazoenezwa na maadui kuhusiana na kadhia ya Lebanon na kusema kama ninavyomnukuu: "Wote mnapaswa kufahamu kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, haiwashinikiza marafiki na waungaji wake mkono, bali inaheshimu matakwa yao sambamba na kusisitizia udharura wa kuchaguliwa rais wa taifa la Lebanon haraka iwezekanavyo." Mwisho wa kunukuu.

1414579

captcha