IQNA – Hafla maalumu ilifanyika katika Msikiti wa Barduşit mjini Pristina, mji mkuu wa Kosovo, kwa lengo la kuwaenzi wanafunzi 80 wa kike wa Qur’ani walioshiriki katika duru za masomo ya Qur’ani Tukufu.
IQNA – Chuo Kikuu cha Jamia Millia Islamia (JMI) mjini New Delhi, India, kilizindua rasmi kongamano kubwa la kimataifa la siku tatu siku ya Jumatano, likiwakusanya wasomi na wanazuoni kutoka pembe mbalimbali za dunia ili kuchambua kwa kina uhusiano hai kati ya mafundisho ya Qur’ani Tukufu na maendeleo ya sayansi ya kisasa.
IQNA – Nakala za Qur'ani zilizoandikwa kwa mfumo wa nukta nundu (Braille) zinasambazwa kwa wageni wanaotembelea Maonesho ya 57 ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo mwaka 2026.
IQNA – Mamlaka ya Fatwa ya Misri (Dar al‑Ifta) imetangaza kwamba matumizi ya programu za akili mnemba (AI), ikiwemo ChatGPT, katika kufasiri Qur’ani Tukufu hayaruhusiwi kisheria.
IQNA – Idadi ya misikiti mipya inayofunguliwa nchini Kazakhstan imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika miaka ya karibuni, ishara ya mwamko wa Kiislamu unaoendelea kushika mizizi katika taifa hilo la Asia ya Kati.
IQNA-Kiongozi mkuu wa Kishia nchini Bahrain amesema katika hotuba kwamba mamilioni ya Wairani wanasimama kidete kulinda uhuru na usalama wa nchi yao kupitia kumuunga mkono Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian amesema kuwa katika ghasia za hivi karibuni, maadui, yaani Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, walilenga kuigeuza Iran kuwa Syria au Libya nyingine,"
IQNA – Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, amefanya mazungumzo na Hissein Brahim Taha, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), mjini Beijing siku ya Jumatatu.
IQNA – Akilaani matukio ya hivi karibuni ya kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu, mwanaharakati wa Qur’ani kutoka Iran ametoa wito wa kuundwa kwa Jumuiya ya Kimataifa wa Maqari wa Qur’ani ambayo miongoni mwa majukumu yake ni kufuatilia hatua za kisheria dhidi ya vitendo hivyo.
IQNA-Mashindano ya Qur’ani kwa wasichana yamefanyika katika mkoa wa Hajjah nchini Yemen, yakionyesha juhudi za kuimarisha elimu ya Qur’ani miongoni mwa wanafunzi wa kike.
IQNA-Lebanon inajiandaa kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani yanayojulikana kama “Al‑Sadiq Al‑Amin,” yatakayofanyika Beirut katika siku za kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani.
IQNA-Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa: "Imam Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni Faqihi Mtawala wetu na sisi hatutabaki kuwa watazamaji mbele ya uchokozi wowote utakaofanywa dhidi ya Iran".
IQNA-Harakati ya Kata’ib Hizbullah ya Iraq (Brigedi za Hizbullah) imetangaza kuwa iko tayari kushiriki katika vita vyovyote vitakavyotokea ili kuilinda Iran, ikitoa wito kwa wanamapambano duniani kote kujiandaa kwa ajili ya hilo.
IQNA – Waziri wa Mambo ya Dini na Awqaf wa Algeria amewakabidhi wanazuoni wa Afrika nakala ya kihistoria ya Qur'ani Tukufu ijulikanayo kama “Rhodosi”, wakati wa kongamano lililofanyika nchini humo kuhusu diplomasia ya kidini.