IQNA

Nchi za Kiarabu zavunja kimya na kulaani jinai za Daesh huko Iraq

19:02 - August 11, 2014
Habari ID: 1438344
Jumiya ya Nchi za Kiarabu hatimaye imetoa tamko la kulaani jinai zinazofanywa na kundi la kigaidi la Daesh baada ya kimya cha muda mrefu.

Kufuatia kikao cha masaa kadhaa katika mji mkuu wa Misri, Cairo, jumuiya hiyo imetoa taarifa na kusema kuwa, jinai zinazofanywa na magaidi wa Daesh ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Taarifa ya Arab League imetaka kuchukuliwe hatua za dharura za kukomesha jinai za kundi hilo la kigaidi sambamba na kulinda haki za wananchi na taifa la Iraq.
Kundi hilo la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu Iraq na Sham kwa kifupi Daesh katika miezi ya hivi karibuni limekuwa likitekeleza jinai za kutisha kaskazini mwa Iraq ikiwa ni pamoja na mauaji ya kinyama, uporaji wa mali za watu, uharibifu wa athari za kidini hususan makaburi ya mitume pamoja na ubakaji. Maelfu ya wakaazi wa maeneo ya kaskazini mwa Iraq wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na jinai za kundi hilo.

1438297

Kishikizo: daesh iraq
captcha