IQNA

Mashindano ya 32 ya Kimataifa ya Qur’ani Iran kuanza 27 Rajab

18:37 - April 16, 2015
Habari ID: 3156549
Awamu ya 32 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanatazamiwa kuanza katika mji mkuu Tehran mnamo 27 Rajab sawa na Mei 15.

Mashindano hayo yataanza sanjari na mnasaba wa Mab’ath (kubaathiwa  au kupewa utume Mtume Muhammad SAW).  Mashindano hayo ya kila mwaka yataendelea kwa muda wa wiki moja hadi Ijumaa tarehe 22 Mei.
Wasomi (maqarii) na waliohifadhi Qur’ani kikamilifu kutoka nchi za Kiislamu na zisizo na Kiislamu watashiriki katika mashindano hayo ya wiki moja. Hassan Danesh ataiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kitengo cha qiraa au kusoma huku Mohammad Mehdi Rajabi akishiriki katika kitengo cha kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hufanyika kila mwaka katika Mwezi wa Rajab chini ya usimamizi wa Shirika la Awqaf nchini.../EM

3096882

captcha