IQNA

Mwislamu Ufaransa alazimishwa kuuza pombe, nguruwe la sivyo duka lake lifungwe

12:30 - August 08, 2016
Habari ID: 3470507
Duka moja la bidhaa halali nchini Ufaransa limeonywa kuwa iwapo haliafiki kuuza pombe na nyama ya nguruwe basi litapokonywa leseni na kufungwa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, duka la Good Price, katika mtaa wa Colombes mjini Paris, linatuhumiwa kuwa ‘halitumikii jamii’ kutokana na uamuzi wake wa kukataa kuuza bidhaa ambazo zimeharamishwa katika Qur’ani Tukufu. Kutokana na msimamo huo wa kuuza bidhaa halali pekee, duka hilo sasa linakabiliwa na tishio la kufungwa.

Meya Nicole Goueta wa Colobes anaripotiwa kutembelea duka hilo yeye binafsi na kuwataka wamiliki wawe na ‘bidhaa anuai’ ikiwa ni pamoja na pombe na nyama zisizo halali.

Mmiliki wa duka hilo, Souleman Yalcin anasema duka hilo linauza bidhaa za jamii ambayo anaihudumia.

Katika mahojiano na gazeti la Le Parisien, amesema anafanya biashara kwa kuzingatia watu ambao anaweza kuwauzia bidhaa zake.

Ufaransa ina karibu Waislamu milioni tano ikiwa ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya Waislamu barani Ulaya.

3460624

captcha