IQNA

Uislamu waenea kwa kasi Madagascar

10:25 - June 05, 2017
Habari ID: 3471007
TEHRAN (IQNA)-Kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la Waislamu nchini Madagascar katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni,idadiya Waislamu nchini Madagascar imeongezeka katika kipindi cha miaka saba kutoka asilimia 10 na kufikia asilimia 15. Wamadagascar waliosolimu wanasema sababu ya ongezeko hilo la wafuasi wa dini ya Uislamu nchini humo, ni kwamba mbali ubora wa kimaanawi, Uislamu pia una mafunzo muhimu ya kijamii.

Maisha ya kijamii ya Waislamu ni mvuto kwa watu wengine na huwapelekea Wasilimu. Aidha waliosilimu Madagascar wanasema hawaaamini propaganda dhidi ya Uislamu huku wakisisitiza kuwa dini hii tukufu haina mafungamano yoyote na harakati za makundi ya kigaidi yanayotekeleza jinai na mauaji.

Halikadhalika waliosilimu Madagascar wanasema Uislamu unapinga kila aina ya mauaji ya kuvizia, kujiripua na ukatili wowote na kinyume chake dini hiyo inasisitizia kuishi na watu wengine kwa amani na udugu, kama ambavyo pia inawalingania watu wa dini nyingine kuingia katikaUislamu kwa amani pasina utumiaji mabavu.

Hayo yanajiri wakati ambao hivi karibuni, Serikali ya Madagascar ilitangaza uamuzi wa kufunga madrassah na taasisi 16 za kufunza Qur'ani nchini humo hatua ambayo imewakasirisha Waislamu nchini humo.

3605551

captcha