IQNA

Vituo vya kufunza Qur'ani Kuwait vyafungwa kwa kuhofia Corona

9:42 - February 29, 2020
Habari ID: 3472515
TEHRAN (IQNA) – Vituo vya kufunza Qur'ani Tukufu nchini Kuwait vimefungwa kwa kuhofia kuenea kirusi cha Corona.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini Kuwait imetoa taarifa na kusema kuanzia Alhamisi, vituo vyote vya kufunza Qur'ani na vituo vya Kiislamu vimefungwa kwa muda wa wiki mbili ili kuzuia kuenea kirusi cha Corona.

Aidha wizara hiyo imetoa wito kwa mahatibu wa Sala ya Ijumaa kuzungumzai umuhimu wa kuchukua tahadhari kuhusu Corona kwa kuzingatia muongozo wa serikali.

Halikadhalika serikali ya Kuwati imefuna shule na vyuo vikuu nchini humo kwa muda wa wiki mbili kutokana na hofu ya kuenea Corona.

Kwa mujibu wa takwimu zaidi ya watu 45 wameabukizwa kirusi cha Corona nchini Kuwait.

3881853

captcha