IQNA

Rais Rouhani: Iran haitakuwa mwanzisjai vita na inafuatilia nyendo za Marekani

14:55 - April 25, 2020
Habari ID: 3472701
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inafuatilia kwa karibu sana nyendo za Marekani na kuongeza kuwa: "Iran katu haiitakuwa muanzishaji wa taharuku na mapigano katika eneo."

Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo leo katika mazungumzo ya simu na Amiri wa Qatar Sheikh Tamim bin Aal Thani ambapo sambamba na kuwasilisha salamu za kheri na fanaka kwa mnasaba wa kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa serikali na taifa la Qatar na pia kwa Waislamu kote duniani, ameelezea matumaini kuwa, mwezi huu utakuwa ni wenye baraka na kheri tele kwa umma wa Kiislamu.

Katika mazungumzo hayo ya simu, Amiri wa Qatar pia naye amewasilisha salamu za kheri na fanaka kwa serikali na taifa la Iran kwa mnasaba wa kuwadia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Amir wa Qatar amesema kuna udharura kwa nchi zote za eneo kufanya kila ziwezalo kuzuia taharuki.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Amir wa Qatar wamesema uhusiano wa Tehran na Doha ni chanya na unazidi kuimarika na wamesisitiza kuhusi udharura wa kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika sekta zote.

3894041

captcha