Kwa mujibu wa tovuti ya Afrigatenews, Sheikh Ahmed bin Ukal amechukua miaka mine kumaliza kazi yake hiyo yenye thamani kubwa. Sheikh bin Ukal ameandika sura zote za Qur’ani Tukufu katika msahafu wenye kurasa 621 kwa kutumia mbinu ya Qalun an-Nafi.
Jitihada za kustawisha harakati za Qur’ani zinaendelea nchini Libya pamoja na kuwa nchi hiyo inaendelea kushuhudia mapigano baada ya muungano wa kijeshi wa NATO kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo na kupelekea kupinduliwa mtawala wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mwaka 2011.