Msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni amesema kuwa mashambulizi hayo ni jibu kwa kutumwa katika vitongoji vya Wazayuni maputo ya moto kutokea Ukanda wa Ghaza.
Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni jana usiku pia zilishambulia eneo la al Brij huko katikati mwa Ghaza.
Vijana wa Kipalestina siku kadhaa za karibuni walirusha vishada vya moto katiak ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu wakilalamikia kuendelea kuzingirwa Ukanda wa Ghaza na Wazayuni.
Ndege za kivita, helikopta, na makombora ya utawala wa Kizayuni katika miezi ya karibuni ziliyashambulia kwa mara kadhaa maeneo mbalimbali huko Ghaza.