Mwaka huu Maulidi inasherehekewa huku Waislamu wakiandamana kulaani hatua ya serikali ya Ufaransa ya kuunga mkono jarida ambalo limemvunjia heshima Mtume Muhammad SAW, ambaye ni Mtume wa Mwisho wa Mwenyezi Mungu. Waislamu wanatumia fursa ya Maulidi mwaka huu kubainisha mahaba na mapenzi yao kwa Mtume Muhammad SAW ambaye ni mbora wa viumbe.