Kituo cha Kuhifadhi Qur’ani cha Makhtoum huandaa mashindano hayo ya kila mwaka. Mwaka huu kutokana na kuenea ugonjwa wa COVID-19, mashindano hayo yatafanyika kwa njia ya Zoom.
Mashindano hayo yatakuwa na kategoria tano ambazo ni kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu, kuhifadhi juzuu 20, kuhifadhi juzuu 15 na kuhifadhi juzuu 10.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Hamid al Khazraji amesema mashindano hayo yanalenga kustawisha kiwango cha kuhifadhi Qur’ani mikoni mwa watu wa marika mbali mbali.