Mhusika katika mchakato huo, Muhammad al Saidi, amesema tartibu zote za Radio Zaitouna kujiunga na Radio ya Kitaifa ya Tunisia zimekamilika baada ya mapatano kutiwa saini Ijumaa.
Hivi sasa Radio Zaitouna inakuwa stesheni ya 11 ya Televisehni ya Kitaifa ya Tunisia. Kwa mujibu wa mapatano yaliyofikiwa Disemba 2020, Radio Zaitouna itaendelea kuwa huru katika kazi zake na haitahusishwa katika migogoro ya kisiasa au mashinikizo kutoka makundi mengine.
Radio Zaitouna ilianzishwa Septemba 2007 kama radio ya kwanza ya Kiislamu nchini Tunisia.