IQNA

Hujjatul Islam Shahriyari

Ukufurishaji ni njama ya Mabeberu, Wazayuni

22:17 - December 04, 2021
Habari ID: 3474640
TEHRAN (IQNA)- Hujjatul Islam wal Muslimin Shahriari amesema itikadi ya Ukufurishaji ni kati ya njama za mabeberu na Wazayuni dhidi ya Uislamu.

Shahriyari ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu ameyasema hayo katika mkutano na wanazuoni wa madhehebu za Shia na Sunni katika mkoa wa Kurdistan, magharibi mwa Iran.

Ameongeza kuwa wakufurishaji wako nje ya Uislamu na kufafania kwamba, kuwa kwa mujibu wa mtazamo wa Kishia haifai kuwakufurisha wale wanaotamka Shahada mbili na kusimamisha sala na kwa msingi huo Mashia hawawakufurishi hata  Mawahhabi.

“Sisi kama Waislamu tunapaswa kufuata mafundisho ya Mtume Muhammad SAW ambaye alisema hatupaswi kumuua mtu anayetamka Shahada,” amesema Hujjatul Islam Shahriyari.

Mwanazuoni huyo wa Kiislamu nchini Iran ameongeza kuwa, vita, ugaidi na ukufurishaji, malumbano pamoja na kutusiana Waislamu ni njama tano ambazo zinachochewa na mababeru na Wazayuni dhidi ya jamii za Kiislamu. Amebaini kuwa Mashia na Masunni wanoeneza matusi na kuvunjiana heshima wanapokea msaada wa kifedha kutoka madola kama vile Uingereza na Marekani.

Aidha amesema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh ni njama iliyoibuliwa na muungano wa Marekani-Uingereza-Israel (Wazayuni) kwa msaada wa Waislamu majahili au wajinga na hivyo kuna haja ya wanazuoni wa Kiislamu kukabiliana na njama hii.

Ukufurishaji kimsingi ni ile itikadi inayofuatwa na pote ndogo la Waislamu ambao huamini kuwa Muislamu yeyyote asiyefuata misimamo au mitazamo yao ni kafiri. Itikadi kama hii imechochea hujuma za kigaidi ambazo hutekelezwa dhidi ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Baadhi ya makundi ya kigaidi yenye kufuata itikadi potovu na ya kibeberu ya ukufurishaji ni pamoja na Boko Haram, Al Shabab na ISIS au Daesh.

5366973

captcha