Kituo cha chanjo ndani ya msikiti huo kimefunguliwa Jumatatu ambapo wakuu wa Huduma ya Kitaifa ya Afya Uingereza (NHS) Ukanda wa Glasgow na Clyde (NHSGGC) wametangaza kupitia Twitter kuwa kutakuwa na wahudumu 45 wa kudunga chanjo katika kituo hicho.
Maafisa wa afya katika eneo la (NHSGGC) wametoa wito kwa wananchi kufika msikitini hapo kupata chanjo kwani kumeshuhudiwa ongezeko la maambukizi ya COVID-19 na hospitali zinakaribia kujaa.
Hayo yanajiri wakati ambao Jumatatu 27 Disemba 2021 watu 98,515 waliambukizwa COVID-19 kote nchini Uingereza ambapo jumla ya maambukizi nchini humo sasa ni milioni 12. Aidha Jumatatu watu 143 walipoteza maisha kutoana na COVID-19 na kufanya idadi ya walipoteza maisha kupindukia 98,515 hadi sasa.