IQNA

Afisa wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu Iran

Marekani ilichinja haki za binadamu kwa kumuua Jenerali Soleimani

21:21 - January 02, 2022
Habari ID: 3474757
TEHRAN (IQNA)- Naibu Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Iran katika Masuala ya Kimataifa ameitaja hatua ya Marekani ya kumuua kigaidi Kamanda Qasem Soleimani kuwa ni sawa na mauaji ya haki za binadamu duniani.

Sayyid Majid Tafreshi amesema katika mkesha wa kuuawa shahidi Haj Qasem Soleimani kwamba: "Hatua hiyo ilikuwa moja ya ukiukwaji mkubwa zaidi wa haki za binadamu duniani."

Tafreshi ameongeza kuwa: "Kesi hii ya kitaifa kwa lengo la kulinda haki za kimataifa, kuimarisha amani na usalama wa kimataifa na kupambana na tabia ya kukwepa mkono wa sheria, haitaachwa ipite hivihivi."

Naibu Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Iran amesema kuwa, mauaj hayo ya kigaidi yaliyofanywa na Marekani si ishara ya sifa nzuri ya kijeshi bali ni kielelezo cha woga ambacho pamoja na kwamba ni uchokozi, vilevile ni ukiukaji wa mamlaka ya Iraq na hata mamlaka ya kujitawala ya Iran.

Tafreshi amesema, Luteni Jenerali Qasem Soleimani alikuwa mwakilishi rasmi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mgeni wa serikali ya Iraq.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi vamizi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Hujuma hiyo ilitekelezwa kwa amri ya rais wa wakati huo wa Marekani, Donald Trump.

Kufuatia jinai hiyo, mnamo Januari 8 mwaka 2020, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilichukua hatua ya kulipiza kisasi kwa kuvurumisha makombora kadhaa dhidi ya kituo cha kijeshi cha Marekani cha Ain al Assad nchin Iraq. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza kuwa bado haijamaliza kulipiza kisasi mauaji ya Shahidi Soleimani na kwamba kuondoka askari wote wa Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia ndiko kutalipiza kisasi damu ya Luteni Jenerali Soleimani.

100131

captcha