IQNA

Rais wa Iran atembelea Qatar, mapatano 14 yatiwa saini

19:46 - February 21, 2022
Habari ID: 3474957
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Qatar leo zimetiliana saini mikataba 14 ya uushirikiano mjini Doha katika nyanja mbalimba katika hafla iliyohudhuriwa na Rais Ebrahim Raisi na Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamesisitiza pia juu ya azma ya nchi zao ya kuimarisha uhusiano katika nyanja mbalimbali huku nchi hizo zikiafikiana kufuta visa baina ya nchi hizo.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake, Rais wa Iran amesema kuwa, taifa hili limethibitisha urafiki wake kwa mataifa yote ya eneo katika kipindi kigumu.

Amesema kuwa, Iran imeibuka na uushindsi katika medani ya vita viwili vya ugaidi na wenzo wa mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa katika uga wa uchumi.

Kwa upande wake Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani ameonyesha kufurahishwa kwake na maafikiano na hatia za ushirikiano zilizotiwa saini na nchi mbili hizo na kueleza kwamba, hiyo ni hatua muhimu mno na ni lazima kufuatilia ili kuhakikisha mikataba hiyo inatekelezwa kivitendo.

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo amewasili mji mkuu wa Qatar, Doha na kulakiwa na kiongozi wa nchi hiyo, Emir Tamim bin Hamad al-Thani.

Katika safari hiyo ya siku mbili Raisi ameandamana na mawaziri kadhaa na inatazamiwa kuwa nchi mbili zitatiliana saini mikataba  ya ushirikiano. Safari hiyo inafanyika kwa msingi wa kuimarisha mawasiliano na nchi za pembeni ya Ghuba ya Uajemi katika mwendelezo wa diplomasia ya ujirani mwema hususan na nchi hizo. 

Kustawisha uhusiano na majirani na nchi za eneo la Magharibi mwa Asia na rafiki ni sehemu ya kipaumbele kikuu cha sera za nje cha serikali ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ebrahim Raisi. Kutokana na eneo lake la kijiografia, Iran inapakana na nchi 15, na hapana shaka kuwa kutumiwa vizuri uwezo wote wa kiuchumi, biashara, viwanda, utamaduni na utalii katika uhusiano na majirani na nchi za eneo hili, kutapelekea kustawishwa uhusiano wa pande mbili na wa pande kadhaa.  

Qatar ni miongoni mwa nchi zinazolengwa na kupewa kipaumbele katika sera ya mambo ya nje za Iran, na historia ya uhusiano wa nchi hizi unaonyesha kuwa, Iran na Qatar zimekuwa na uhusiano mkubwa na unaozidi kukua na kustawi. Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Qatar ni sehemu ya jitihada za Tehran za kupanua na kuimarisha uhusiano, na safari ya Qatar ni awamu ya kwanza ya ziara ya Rais wa Iran katika nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi; jambo ambalo linaonesha umuhimu maalumu wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Safari ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Qatar na mikataba muhimu ya pande mbili itafungua ukurasa mpya katika ujirani mwema, na Iran daima imekuwa ikitoa kipaumbele katika kupanuka uhusiano na majirani zake na nchi za eneo la Asia Magharibi katika siasa zake za nje.

 

4037939

captcha