IQNA

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje

Azma ya Iran ya kuwa sauti ya ulimwengu wa Kiislamu

22:16 - March 23, 2022
Habari ID: 3475068
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu imejitolea kwa dhati kuendelea kupaza sauti ya ulimwengu wa Kiislamu na mataifa yanayodhulumiwa duniani.

Saeed Khatibzadeh amesema hayo katika mahojiano na shirika la habari la IRNA akiwa mjini Islamabad nchini Pakistan, alikoenda kushiriki Kikao cha 48 cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).

Amesema nchi za Kiislamu, kuanzia Yemen hadi Syria na Palestina inayokaliwa kwa mabavu zinakabiliwa na changamoto za kutisha, na kusisitiza kuwa OIC ina wajibu wa kuyatafutia ufumbuzi matatizo hayo.

Khatibzadeh amebainisha kuwa, OIC ndiyo jumuiya muhimu zaidi ya ulimwengu wa Kiislamu duniani, na ambayo imekusanya kijogfaria mataifa kadhaa ya Waislamu.

 

Kadhalika Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameyakosoa baadhi ya madola akisisitiza kuwa, mataifa yote ya Kiislamu yanapaswa kufungamana na kadhia ya Palestina, ambayo ni moja ya misingi mikuu ya kuanzishwa jumuiya kama hizo za Kiislamu.

Ameongeza kuwa, OIC inapaswa kuyaleta pamoja mataifa ya Kiislamu na kupigania umoja wao, akisisitiza kuwa hatua ya karibuni ya kuanza kuimarika uhusiano wa Iran na Saudia ni kwa maslahi ya mataifa yote ya eneo.

 

3478256

captcha