IQNA

Wasomi: Kazi za kiutamaduni zinahitajika ili kukabili ukufurishaji

13:06 - April 14, 2022
Habari ID: 3475127
TEHRAN (IQNA)- Katika cha mtandaoni kilichoandaliwa na Shirika la Habari la IQNA, wataalamu waMEsisitiza kwamba kazi zaidi ya kitamaduni inahitajika kufanywa ili kukabiliana na makundi ya kitakfiri au wakufurishaji kama vile Daesh (ISIS au ISIL).

Mkutano wa mtandao uliandaliwa na IQNA siku ya Jumanne ukiwa na jina la "jukumu la uhusiano wa kina kati ya Iran na Afghanistan katika vita dhidi ya fikra za ukufurishaji".

Mohammad Ebrahim Shariati, mchapishaji kutoka Afghanistan, Mohsen Pakaeen, mkuu wa zamani wa kamati ya Afghanistan katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, na Abdolshahid Sagheb, mtafiti na mwandishi wa habari wa Afghanistan walihutubia kikao hicho kilichofanyika wiki moja baada ya shambulio la kisu dhidi wasomi wa kidini katika Haram Takatifu ya Imam Ridha AS mjini Mashhad, nchini Iran ambapo wasomi wawili wa Kiislamu waliuawa shahidi na mmoja kujeruhiwa.

Akizungumzia chimbuko la utakfiri, Shariati alibainisha kuwa moja ya sababu za kuibuka makundi hayo yenye misimamo mikali ni propaganda zinazofanywa na baadhi ya makundi ya Kiislamu dhidi ya kila mmoja wao.

Baadhi ya wanaojiita vikundi vya Kiislamu sasa hata wanashirikiana na Wayahudi kuwadhoofisha Waislamu wengine, alisema, na kuongeza, "Tunapaswa kutafuta suluhisho kwa hili kupitia wasomi wetu katika seminari za Kiislamu, vyuo vikuu na vyombo vya habari."

Vile vile ameashiria ulazima wa wanazuoni wa Kiislamu kueleza na kudhihirisha  rehema ya Uislamu kwa walimwengu.

Akiashiria historia ndefu ya uhusiano kati ya watu wa Iran na Afghanistan, Pakaeen alisema kuwa baadhi ya maadui wanataka kuzusha mifarakano kati ya nchi hizo mbili.

Amesema mashambulio ya hivi karibuni mjini Mashhad hayahusiani na taifa la Afghanistan bali ni wale wenye fikra za ukufurishaji na  wao si Shia wala Sunni. "Chokochoko hii ina malengo ya kisiasa na inaungwa mkono na idara za kijasusi za nchi ambazo hazitaki uhusiano mzuri kati ya Iran na Afghanistan."

Suluhu muhimu zaidi ya kukabiliana na ukufurishaji, aliendelea, ni kupitia kazi za kitamaduni. Kwa kutumia diplomasia yenye nguvu, serikali zinapaswa kuangazia mambo yanayofanana na kudhoofisha athari za propaganda za ukufurishaji kupitia programu za kitamaduni na elimu.

Shambulio la mtu aliyedanganywa dhidi ya maulama watatu kwenye Haram ya Imam Ridha (AS) halimaanishi makabiliano kati ya mataifa mawili ya Iran na Afghanistan, alisema.

Moja ya hatua ambazo Marekani ilitekeleza kabla ya kuondoka Afghanistan ni kuhamisha Daesh (ISIS au ISIL) hadi kaskazini mwa nchi hiyo na hili ni mojawapo ya matatizo muhimu zaidi kwa nchi hiyo katika siku zijazo, Parkaeen alisema.

Kwa upande wake, Sagheb alisema shambulio la hivi karibuni la mapanga linaonyesha kuwa baadhi ya maadui waliojificha wanataka kuigeuza Afghanistan kuwa eneo jipya la makundi ya Daesh na Takfiri na kituo cha kusafirisha mawazo hayo.

Alitaja kusambaratika kwa jeshi hilo la Afghanistan, umaskini, kushindwa kuanzisha serikali shirikishi, chuki za kimadhehebu na kikabila, na waungaji mkono wa kigeni kuwa sababu za ukuaji wa makundi yenye itikadi kali.

4049129

captcha