IQNA

Msikiti wahujumiwa Ufaransa kabla ya Macron kuapishwa

19:06 - May 07, 2022
Habari ID: 3475217
TEHRAN (IQNA)- Msitiki umehujumiwa katika mji wa Metz, kaskazini mashariki mwa Ufaransa siku moja kabla ya Emmanuel Macron kuapishwa kuendelea kuwa rais wa Ufaransa.

Msikiti huo unasiamiwa na Muungano wa Kiislamu-Uturuki wa Masuala ya Kidini (DITIB) na uliharibiwa baada ya kuvurumishiwa mabomu matatu aina ya Molotov na watu wasiojulikana.

Mwenyekiti wa msikiti huo Ali Durak amesema hujuma hiyo imejiri Ijumaa alfajiri ambapo madirisha ya msikiti huo yaliteketezwa moto.

Amesema msikiti huo kwa kawaida huendesha shughuli zake kwa kushirukiana na raia wote wa Ufaransa katika mji huo sambamba na kutoa misaada bila kujadili dini.

Kamati ya Jumuiya za Kiislamu Ufaransa imetoa taarifa na kusema kumeshuhudiwa ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu nchini humo. Ameongeza kuwa, Chuki dhidi ya Waislamu zimedhihirika zaidi wakati wa uchaguzi wa hivi karibuni wa Ufaransa.

Shambulizi dhidi ya msikiti huo limejiri siku moja kabla ya Emmanuel Macron kuapishwa kuendelea kama rais wa Ufaransa baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa hivi karibuni.

Serikali ya Macron imekuwa mstari wa mbele kuchukua hatua dhidi ya Waislamu na inatazamiwa kuwa ushindi wake utapelekea Waislamu waendelee kubanwa na kubaguliwa zaidi Ufaransa.

3478796

Kishikizo: ufaransa waislamu macron
captcha