Rais Raisi aliongeza kuwa: "Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Iran iligeuka na kuwa kimbilio la watu wanaodhulumiwa duniani.."
Leo 14 Khordad kwa mujibu wa Kalenda ya Hijria Shamsia sawa na tarehe 4 Mfunguo Pili Dhul-Qaadah mwaka 1443 Hijria, mwafaka na tarehe 4 Juni 2022 Miladia ni siku ya kukumbuka kuaga daunia Imam Khomeini -Mwenyezi Mungu Amrehemu- Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran Press, katika hotuba yake, Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwaokoa waliodhulumiwa na waliodhoofishwa katika ardhi ni moja ya nukta muhimu sana katika fikra za kisiasa za Imam Khomeini (MA). Aliongeza kuwa watu wote waliodhulumiwa duniani walimtazama Imam kama kiongozi wao.
Akiendelea na hotuba yake, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliashiria kauli ya Imam Khomeini MA aliposema: 'Marekani haina ubavu wa kufanya chochote' na kuongeza kuwa, leo tunashuhudia msemaji wa Ikulu ya White House akitangaza wazi kuwa mashinikizo ya juu kabisa ya Marekani dhidi ya Iran yamefeli.
Raisi ameendelea kwa kubaini kuwa wanasiasa duniani ni wengi lakini siasa bila kumcha Mwenyezi Mungu huibua msiba kwa mwanadamu na kuongeza kuwa, siasa bila umaanawi ndio sababu ya Wapalestina kudhulumiwa kwa zaidi ya miaka 70 na pia ni chanzo cha kushuhudiwa mashindano ya silaha za atomiki duniani.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, mustakabli wa Iran ni mwema na uliojaa nuru na kuongeza kuwa: "Nukta hii inapatikana katika miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Imam Khomeini MA."
3479165