Roboti imetumika kusambaza nakala za Quran huku mahujaji wakimaliza safari yao ya Hajj huko Makka.
Akitoa maelezo juu ya kifaa hicho, Naibu Katibu Mkuu wa Rais wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina Badr bin Abdullah Al-Firaih alisema roboti hiyo ambayo hupita kwa urahisi katikati ya umati wa watu, ina uzito wa kilo 59 na kasi inayoweza kudhibitiwa ya mita 1.2 - 5 kwa sekunde na uwezo wa kubeba kilo kumi.
Takriban mahujaji milioni moja kutoka nchi mbalimbali walifanya ibada ya Hija mjini Mecca mwaka huu, baada ya kufanya ibada hiyo na idadi ndogo ya mahujaji katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kutokana na janga la virusi vya corona.
3479670